30 Desemba 2024 - 05:47
MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA - SOMO LA 1: KUFIKIRIA, TAAMULI

Kuujaza ubongo wa mtu kwa kanuni za kisayansi, mantiki na kifalsafa, au na elimu yoyote itakuwa na athari ndogo sana hadi hapo itakapokuwa kwa misingi ya fikara sahihi, mtazamo wazi wa ulimwengu na kuzitambua misingi ya maisha ya mwanadamu.

Uwe tahadhari! Elimu isiyo ambatana na ufikiriaji, haina faida. Uwe tahadhari! Usomaji wa Qur'an Tukufu iwapo hautakuwa na ufikiriaji, basi hautakuwa na maana! Uwe tahadhari! 'Ibada isiyo na fikara ndani mwake, haina athari yake.  Al-Kaafi ,J.1, Uk. 36; Tuhfatul 'Uquul

Maelezo mafupi: 

Kuujaza ubongo wa mtu kwa kanuni za kisayansi, mantiki na kifalsafa, au na elimu yoyote itakuwa na athari ndogo sana hadi hapo itakapokuwa kwa misingi ya fikara sahihi, mtazamo wazi wa ulimwengu na kuzitambua misingi ya maisha ya mwanadamu.

Ama usomaji wa Qur'an Tukufu utakuwa na athari ndogo iwapo haitaambatana na uchambuzi na kuzizingatia na kuzifikiria hizo Ayah zake, 'Ibada ambayo haina nuru ya ufikiriaji na busara ni sawa na mwili usio na roho, na kukosa athari za elimu ya hali ya juu.

  Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho "MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA" - Ayatullah Makarim Shirazi